Ahukumiwa Miaka 92 Jela Kisa Bangi - Mtwara
Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu imemuhukumu kifungo cha miaka 92 jela Salumu Yohana Mkonya (54) Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Mnazimmoja, kwa makosa ya kupatikana na mbegu na majani ya mimea ya dawa za kulevya aina ya bangi, misokoto ya dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na kupatikana na pombe haramu ya moshi.
Akitoa taarifa ya kesi ambazo Polisi imepata mafanikio Mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akihifadhi dawa za kulevya pamoja na pombe haramu ya moshi katika nyumba yake kwa lengo la kujipatia kipato.
Tembelea website yetu kila wakati ili uwe Wa kwanza KUPATA kila habari inayotrend hapa Tz na nchi nyingine kwa wakati
SHARE THIS POST PLEASE