Hamisa Mobetto Na Azizi Ki Watangaza Siku ya Ndoa Yao

Hamisa Mobetto Na Azizi Ki Watangaza Siku ya Ndoa Yao
Hamisa Mobetto Na Azizi Ki Watangaza Siku ya Ndoa Yao
 
Hamisa Mobetto Na Azizi Ki Watangaza Siku ya Ndoa Yao

Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Yanga ya Dar es Salaam, Stephane Aziz Ki, pamoja na mwanamitindo, muigizaji, na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Hamisa Mobetto, hatimaye wameweka hadharani tarehe ya ndoa yao, ambayo wameiita MissaKi2025.

Mtangazaji maarufu na mmiliki wa Zamaradi TV, Zamaradi Mketema, leo Februari 10, 2025 ametangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa siku ya mahari itakuwa Februari 15, 2025 na ndoa itafungwa Februari 16, mwaka huu.

Aidha Zamaradi amesema sherehe rasmi kwa ajili ya maharusi hao itafanyika Februari 19 mwaka huu.

Hamisa Mobetto Na Azizi Ki Watangaza Siku ya Ndoa Yao


Hivi karibuni, wawili hao walifichua uhusiano wao wa kimapenzi baada ya kuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu.

Mchokonozi alikuwa ni Haji Manara siku moja ya ‘Siku ya Mwananchi’ alipomtoa Mobeto jukwaani na kumuambia akajiunge na Azizi K wakati wa utambulisho na wanayanga kulipuka kwa furaha kuwashangilia.

Awali, baada ya utambulisho huo uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wawili hao walikuwa wakikanusha uvumi wa kuwa wapenzi huku wakiepuka maswali ya mashabiki na vyombo vya habari kuhusu ukaribu wao.

Hata hivyo, sasa si siri tena baada ya kushiriki picha za pamoja wakifurahia mapumziko ya kifahari (vacation) nchini Dubai na tayari wametengeneza tangazo linalohusu siku ya ndoa yao na inasambaa kwenye mitandao ya kijamii. Azizi Ki ni mtu wa Burkina Faso wakati Mobet oni Mbongo


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post