Meneja LBL anaswa Biashara za Upatu Mitandaoni

Meneja LBL anaswa Biashara za Upatu Mitandaoni


 Meneja LBL anaswa Biashara za Upatu Mitandaoni 

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watuhumiwa watano akiwemo Meneja wa Kampuni ya LBL Gerald Masanya ,31, kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali chochote ambapo ni kinyume na taratibu za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Wilbert imeeleza baada ya kupata taarifa za uwepo wa Kampuni ya LBL Mbeya Media Limited kuwa inajihusisha na biashara ya upatu mtandaoni walianza kufuatilia kwa kushirikia na Maofisa kutoka Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya na idara nyingine ambapo walifika maeneo ya Mwanjelwa na kuwakamata watumiwa hao.

Taarifa hiyo imewataja watuhumiwa hao ni Gerald Masanya ,31, ambaye ni Meneja wa Kampuni ya LBL-Mbeya, mkazi wa Nsalaga, Saphina Mwamwezi ,23, ambaye ni sekretari na mkazi wa Ituha, Edda William ,29, mkazi wa Uwanja wa Ndege wa Zamani, Yohana Mkinda ,29, mkazi wa Tukuyu pamoja na Macrine Sinkala 23.


#LBL #Tanzania #eatv #itv #startv #wasafitv #wasafifm #cloudsfmtz #cloudstv

#azamtv #azam2tv #azamsports


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post