Phina Atangaza Kuachana na Meneja Wake - D Fighter
Mwimbaji wa Bongofleva, Phina ametangaza kuachana na aliyekuwa meneja wake kwa muda mrefu, D Fighter.
Katika taarifa yake kwa umma, Phina amesema ameamua kuachana na meneja huyo kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wake, phina ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2018, akifanya kazi na D Fighter ameshinda tuzo nne za Muziki (Tanzania) TMA.