Mtengeneza maudhui mitandaoni, Zerobrainer kutokea Tanzania ameshinda tuzo ya Sports Creator of the Year TikTok Awards 2024 katika tuzo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2025 Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Baada ya ushindi huu, Zerobrainer anaweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo.
Zerobrainer amejizolea umaarufu mkubwa hasa katika mtandao wa TikTok kutokana na aina ya maudhui yake ya michezo anayotengeneza na ndiye Mtanzania mwenye wafuasi wengi zaidi katika mtandao huo akiwa nao milioni 12.9.