Ajali mbaya imetokea eneo la Gongolamboto mwisho, kwenye kilima cha kuingia Pugu Sekondari, na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Chanika (OCD), Awadh Mohamed Chiko.
Kwa mujibu wa mashuhuda, daladala la aina ya Eicher lilitanua na kufuata upande wa gari la OCD Awadh, ambaye alikuwa akiendesha Toyota Prado, na kusababisha ajali hiyo mbaya
Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali na hatua zinazochukuliwa na vyombo vya usalama zitaendelea kufuatiliwa.
OCD Wa Chanika Atazikwa Makabiri ya kisutu Tar 18/03/2025
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika SP Awadh Chiko unatarajiwa kuzikwa kesho Machi 18, 2025 katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa taratibu za kijeshi.
SP Awadhi Chico amefariki Dunia leo Majira ya Asutbuhi kufuatia Ajali ya Gari iliyotokea eneo la Pugu Sekondary baada ya Basi aina ya Eicher kugongana na gari la SP Awadh aina ya Prado wakati alipokuwa akielekea katika majukumu yake ya kila siku.
Kabla ya kuzikwa hapo kesho, mwili wa Marehemu SP Awadh utaswaliwa katika msikiti wa Akachube uliopo kijitonyama na kwa sasa msiba upo Nyumbani kwakwe, Kijitonyama Mtaa wa Bukoba