Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

Baada ya kusota Mahabusu kwa takribani wiki tatu, Mwigizaji Joyce Mbaga maarufu Nicole Berry ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni baada ya kutimiza masharti ya dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mahakamani hapo ambapo imeelezwa Mahakamani kuwa Nicole amedhaminiwa kwa hati ya nyumba yenye thamani ya Tsh. milioni 100.
Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

Mbali na Nicole, mwingine aliyeachiwa kwa dhamana ni Mshtakiwa mwenzake Rehema Mahanyu (31) ambapo wawili hao walipandishwa kizimbani March 10, 2025 wakikabiliwa na mashtaka ikiwemo kupokea Tsh. milioni 186.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Wawili hao, wameachiwa kwa masharti ya dhamana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemarila, anayesikiliza kesi hiyo, baada ya kutimiza masharti haya ya dhamana.
Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

Nicole amedhamiwa kwa hati ya nyumba yenye thamani ya Tsh. milioni 100 lakini aliyemdhamini bado hajawekwa wazi, huku mwenzake Rehema akidhaminiwa na Ramadhan Juma pamoja na Joyce Isdon ambao waliwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Tsh. milioni 57 milioni.

Kesi ya Nicole na mwenzake inatarajiwa kurudi Mahakamani hapo, March 24, 2025 ambapo leo March 17, 2025 walifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya dhamana ambapo miongoni mwa makosa yao katika shtaka la kwanza wanatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu , wanatuhumiwa kwa miezi hiyo na miaka hiyo wakiwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam waliendesha biashara ya kihalifu au jinai, kwa lengo la kujipatia faida kutoka kwa jamii na kupokea amana au miamala bila kupata leseni kutoka BOT.

Katika shtaka la pili wote wanatuhumiwa kati ya July 2024 na March 2025 wakiwa eneo lisilofahamika ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam walipokea amana ya TSh 185,515,000 kutoka kwa jamii bila kuwa na leseni na katika shtaka la tatu waliendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni ya malipo inayotolewa na BoT.

Nicole Berry Alivyotolewa Jela Kwa Dhamana ya Nyumba ya Milioni 100

 

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post