TFF Yaufungia Uwanja Wa Tabora United
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi unaotumiwa na Tabora United katika michezo ya Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kanunua kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni ya klabu.